Rasmi mmiliki wa Leicester City amefariki kwenye ajali ya helkopta
Klabu ya Leicester City imethibitisha kuwa mmliki wao Vichai Srivaddhanaprabha ,60, ni mmoja wa watu watano waliofariki katika ajali ya helikopta iliyotokea juzi jumamosi katika viunga vya uwanja wa King Power baada ya mechi kati Leicester City kumalizika.
Polisi wamesema kuwa watu wengine wanne waliofariki kwa ajali hiyo ni wasaidizi wake wawili Nursara Suknamai na Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na abiria mmoja, Izabela Roza Lechowicz.
Binti wa tajiri huyo Voramas, anaripotiwa hakuwepo kwenye helikopta hiyo kama taarifa za awali zilivyokuwa zinasema.