De Gea amwondoa wasiwasi Mourinho
Huku klabu ya Manchester United ikiwa ipo katika kiwango kibovu kutokana na kushindwa pata matokeo mazuri na yasiyo ya kuridhisha.
Kipa David de Gea amesema kwa sasa anafikiria zaidi kuipatia timu yake ushindi na sio kuhusu mkataba wake. Kipa huyu ambae mkataba wake na klabu hii ya Old Trafford unafikia tamati katika majira yajayo ya joto mazungumzo juu ya mkataba wake tayari yamekwisha anza miezi kadhaa hadi sasa.
Akizungumza na kituo cha SkySports nchini Uingereza David de Gea alisema anajitahidi kuepuka kuongelea masuala ya mkataba wake ili apate kuweka mawazo yake katika kutafuta matokeo mazuri kwa timu yake na sio kuhusu mkataba wake sababu matokeo ndio kitu muhimu zaidi kwa sasa.
“Kama tulivyosema nimekuwa hapa kwa misimu mingi, msimu wa nane katika klabu kwa sasa. Nipo na furaha na ninapata /hamasa/ toka kwa mashabiki na kila mtu ndani ya klabu.”
Kipa huyu amekuwa katika kiwango kisicho cha kuridhisha ikilinganishwa na msimu uliopita alipokuwa katika kiwango cha hali ya juu. Amejitete kwa kueleza kuwa wanaweka jitihada sababu wanacheza kila baada ya siku tatu ama nne hivyo kuhitaji muda zaidi wa kujiweka sawa mazoezi na sio mambo mengine.
“Ni kuweka mawazo katika yale yaliyo ya msingi kwa sasa ambayo ni timu. Kupata ushindi, kufanya vyema mazoezi na kuwa katika hali nzuri na hapa mengine yatapatikana.”
“Huitaji kufikiria sana mambo yasiyo muhimu katika soka na kupata points ambazo zinahitajika ndio swala la msingi kwa sasa.”
Kocha Jose Morinho ambaye nae muafaka wake katika klabu hiyo upo katika sinto fahamu toka kwa mashabiki amekasema hana imani kama kipa huyo atasaini mkataba mpya na klabu hiyo ila ni vyema klabu ikahakiki anabaki.