Simba, Yanga na Azam kupumzika kupisha maandalizi Taifa Stars
Mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazozihusu timu za Azam FC , Simba SC na Young Africans zilizopangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Novemba zimeahirishwa kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea mechi dhidi ya Lesotho itakayochezwa Novemba 18, mwaka huu kwaajili ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mechi hizo ni kati ya
African Lyon Vs Yanga iliyopangwa kufanyika Novemba 7
Simba SC Vs KMC FC iliyopangwa kufanyika Novemba 8
Azam FC Vs Mbao FC iliyopangwa kufanyika Novemba 8
Mezi zote hizi kuchezwa jijini Dar es Salaam, Tanzania.