Maurcio Pochettino atajwa kutua Real Madrid
Real Madrid wanatajwa kutaka kumchukua kocha wa Tottenham Hotspur Maurcio Pochettino aende kuchukua Julen Lopetegui ambaye amekuwa na msimu mbaya tangu kuichukua timu hiyo majira ya kiangazi.
Kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte pia anatajwa kuwa ndiye anaongoza katika mbio za kuchukua kibarua hicho.
Real wameripotiwa kuwa wanatazama kama kuna uwezekano wa kumpata Poch kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho ya kuhusu kuwa kocha mpya.
Wakati huo huo, kaka wa kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ambaye pia ni wakala wale, Daniele amesema kuwa hawajafanya mawasiliano yoyote na Conte.
“Antonio yupo katika likizo. Hajapokea simi yoyote kutoka Real Madrid. Ndio, Real ni timu kubwa lakini hakuna mawasiliano yoyote“ amesema Daniele.