Smalling ajitia kitanzi Man United
Beki wa Manchester United Chris Smalling amesaini kandarasi mpya katika klabu hiyo itakayomfanya akae hapo mpaka mwaka 2022.
Mchezaji huyo,29, ambaye amecheza zaidi ya mechi 300 katika klabu hiyo tangu atue akitokea Fulham mwaka 2010,amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu.
“ Ninafuraha kujua meneja na klabu wapo na mimi, ninategemea kuwalipa “ alisema mchezaji huyo baada ya kumwaga wino.
Kocha wake Jose Mourinho alisema: “ Ninafurahi Chris amesaini mkataba mpya . Chris amekuwa na klabu hii kwa miaka mingi na sasa ni moja ya wachezaji wakubwa katika kikosi “