Vita ya Klopp na Mourinho Anfield leo
Ni vita ya wapinzani wawili wa jadi leo katika dimba la Anfield. Majogoo wa jiji Liverpool wakiwakaribisha Man United ambao wapo katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, wakipitwa pointi 16 na vijana wa Jurgen Klopp.
Majogoo hao ambao wamefanikiwa kufuzu hatua ya mtoano klabu bingwa Ulaya baada ya kumfunga Napoli katikati ya wiki hii, wanataka ushindi ili kurudi kileleni ambapo Manchester City wameshika usukani.
Liverpool haijapoteza mchezo wowote dhidi ya Man United katika uwanja wa Anfield tangu mwaka 2013, ingawa pia hawajawafunga katika ligi kwenye mechi za nane za ligi zilizopita.
Man United watashuka wakiwa na hasira ya kupoteza mchezo wao uliopita, na endapo watashinda leo, itakuwa ni timu ya kwanza kushinda mechi dhidi ya Liverpool katika ligi msimu huu.