Simba yaangukia pua Zambia
1Baada ya kuingia kwa kishindo katika hatua ya kwanza ya ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo walikuwa jijini Kitwe kuwavaa Nkana FC katika mchezo wa raundi hiyo ya kwanza.
Mabingwa hao wa Tanzania wameondoka vichwa chini katika mchezo huo baada ya kupewa kichapo cha goli 2-1, magoli ya Nkana fc anayoichezea Mtanzania Hassan Kessy yamewekwa wavuni na Ronald Kimpamba dakika ya 27 na Kelvin Kimpamba dakika ya 56.
Bao pekee la Simba limefungwa na nahodha wao John Bocco kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 73, na hivyo kuleta matumaini kwa kupata goli la ugenini kwa Simba ambao lengo lao ni kufika hatua ya makundi wa ya michuano hiyo.
Mechi ya marudiano itapigwa jijini Dar es salaam wikiendi ijayo.