Mourinho kama Sir Alex wote wanauwezo wa kupindua meza kibabe
Winger wa zamani wa Manchester UTD Luis Nani ameelezea imani yake kwa kocha Jose Mourinho licha ya mambo kuwa kama hayaendi sawa.
Ingawa kumekuwa na maneno maneno kuhusiana na mahusiano mabaya kati ya wachezaji na kocha Jose Mourinho ila bado ninaamini Mourinho ndio kocha sahihi pale, yeye pamoja na Sir Alex wamejaliwa kipaji kikubwa kwenye ufundishaji na wote wawili wanasifa moja ya kuweza kuusoma mchezo na kubadilisha matokeo hata katika nyakati ngumu, alieleza Luis Nani kupitia mtandao wa Goal