Mo Salah ashinda tuzo ya BBC ya Mchezaji bora wa Afrika mwaka 2018
Mshambuliaji wa kikosi cha Misri na Liverpool Mohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2018
26, Mo Salah amewashinda Medhi Benatia, Kalidou Koulibaly, Sadio Mane pamoja na Thomas Partey na kuchukua tuzo hii kwa mara ya pili mfululizo.
Ni furaha kubwa kushinda tuzo hii kwa mara nyingine, nimefurahi sana na ningependa kushinda tena mwakani alisema Mo Salah
Kwa mwaka 2019 kitu chake kikubwa ni kushinda makombe akiwa pamoja na klabu yake ya Liverpool, Ninataka kuongeza bidii na kuisaidia timu yangu nikiwa na wenzangu kuweza kushinda makombe msimu huu na Liverpool aliongeza Mo Salah
Washindi 5 wamiaka ya karibuni waliowahi kushinda tuzo hii
2017 : Mohamed Salah (Liverpool na Misri)
2016: Riyad Mahrez (Leicester City na Algeria)
2015: Yaya Toure (Manchester City na Ivory Coast)
2014: Yacine Brahim (Porto na Algeria)
2013: Yaya Toure (Manchester City na Ivory Coast)