MWINYI ZAHERA AMTEMA BENO KAKOLANYA YANGA SC
Jana saa chache baada ya mdau wa Yanga Cyprian Musiba kutangaza na kumpatia Tsh Milioni 2 milanda mlango wa Yanga Beno Kakolanya ili asitishe uamuzi wake wa kugoma kucheza na kwenda kuongeza nguvu katika kikosi cha Yanga kinachowania taji la Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amegoma kurudi kwa mchezaji huyo katika kikosi, kwa madai ya kuwa kuna wachezaji wengi wanaodai ila wamevumilia hivyo, kama atamruhusu Kakolanya aungane na timu na wale wengine wakigoma vipi? Mdau atawaita awapatie pesa ili wacheze.
Zahera alifika mbali zaidi na kueleza kuwa kama Kakolanya anadai pesa zake za usajili hata mlinda mlango wa Congo Kindoki na Heritier Makambo nao bado wanadai ila wamevumilia na wanaendelea kucheza na kuipambania timu, Kakolanya anadai Yanga Tsh Milioni 15 za usajili lakini amepewa Tsh Milioni 2 na Cyprian Musiba ili aendelee kucheza wakati wakizitafuta Tsh milioni 13 zake.
“Watu wanatuma mavideo kama wamempa pesa sasa mimi nawauliza hawa watu, wengi hapa wanadai sasa kesho kama na hawa wengine wakigoma wakaacha mazoezi huyo mtu atawaita na kuwapa pesa Tsh milioni 2 mrudie mazoezi? Hivyo mimi ndio naita vitu vya hovyo, siwezi kukubali vitu vya hivyo, Beno aliandika barua kuwa anavunja mkataba na timu yetu”alisema Mwinyi Zahera
Hata hivyo Yanga bado wanongoza Ligi kwa kuwa na alama 41 baada ya kucheza michezo 15, Azam FC ikiwafuatia kwa wakiwa na alama 40 wakiwa wamecheza michezo 16 na Simba nafasi ya tatu wakiwa na alama 27 na viporo vitatu dhidi ya Yanga wanaongoza na vinne dhidi ya Azam FC waliopo nafasi ya pili.