OWEN ASIMAMA KUMTETEA POGBA DHIDI YA MOURINHO
Nyota wa zamani wa vilabu vya Liverpool na Manchester United Michael Owen ameonekana kuingilia kati ishu iliyokuwa ikiendelea kuhusiana na tuhuma za kocha wa Manchester United Jose Mourinho kuhusiana na uwezo wa kiungo wake Paul Pogba.
Mourinho na Pogba wamekuwa hawaelewani mara kadhaa imewahi kuripotiwa hivyo lakini sababu kubwa inaelezwa kuwa Jose Mourinho anamtuhumu Pogba kuwa sehemu ya timu yake kufanya vibaya, kwa sababu amekuwa hamtumii inavyotakiwa.
Michael Owen amesikika akisema kuwa kama kiungo wa kifaransa Paul Pogba angekiwa anacheza chini ya kocha wa sasa wa Manchester City Pep Guardiola au kocha wa sasa wa timu yake ya zamani ya Liverpool Jurgen Klopp, basi kiungo huyo angetangazwa kama moja kati ya wachezaji bora wachache duniani
“Nasikitishwa sana nikimuangalia (Pogba) ni bora zaidi ya tunachokiona kila wiki anakuwa nje ya uwanja , kwa kiasi kikubwa nipo upande wake sifikiri kwa namna timu inavyocheza au kocha anavyomtumia anatengeneza kupata kitu bora kutoka kwake, Kama (Pogba) angekuwa anacheza chini ya Guardiola au Klopp basi angekuwa miongoni mwa wachezaji bora wachache hapa duniani”alisema Owen
Kauli hiyo ni wazi inaashiria kuwa Michael Owen yuko upande wa Pogba kwa sakata linaoendelea kati ya Pogba na Mourinho japo mbele ya wandishi wa habari wawili hao huwa wanadaiwa kuwa wapo sawa ila chini kwa chini kama kuna kitu cha siri hivi, Pogba alirudi kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Valencia wa Ligi ya Mabingwa jana lakini alikuwa amewekwa benchi na Mourinho katika michezo miwili iliyopita.