KINGSLEY COMAN YUKO TAYARI KUACHA SOKA
Kinda wa FC Bayern Munich ya nchini Ujerumani Kingsley Coman ameonesha dhamira yake ya kushindwa na uvumilivu wa kufanyiwa upasuaji mara mbili mfululizo katika kipindi kifupi, upasuaji ambao umekuwa ukihusisha sehemu moja pekee.
Mwezi huu Coman ‘22’ amefanikiwa kurudi uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa upasuaji wa pili wa enka ya kushoto toka alipoumia mechi ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Hoffenham, hivyo kusababisha kurudi tena nje ya uwanja akiwa ndio alikuwa anarejea tena kutoka kwenye majeruhi.
Coman kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Hoffenham aliumia tena akiwa ndio ametoka kupona jeraha hilo la goti kutokana na kuumia mwezi wa Februari mwaka huu na kufanyiwa upasuaji, hivyo mwanzo wa msimu akaumia tena kwa kiwango cha kuhitaji upasuaji, Coman amesema akipata jeraha kubwa tena likahitaji upasuaji ataachana na soka na kustaafu kwani anaamini miguu yake haitakuwa imetengezwa kwa kazi hiyo.
“Nimekuwa na msimu mgumu sana na nimekuwa nikiumia, namatumaini sitapitia tena wakati mgumu, kiukweli inatosha sitokubali upasuaji wa tatu, hiyo itaashiria kuwa mguu wangu haujatengenezwa kwa kazi hii na nitatafuta kazi nyingine”>>> alisema Kingsley Coman