Kwa kauli hii Klopp na Liverpool haondoki leo
Pamoja na kuwa klabu ya Liverpool ya Uingereza Jumanne ya Desemba 11 usiku itakuwa Anfield kucheza dhidi ya Napoli ya nchini Italia, kocha wao Jurgen Klopp amezima tetesi za uwezekano way eye kwenda kufanya kazi Italia.
Klopp wengi walikuwa wakiamini anavutiwa na Italia ila mwenyewe amekiri kuwa anachokipenda Italia ni chakukal chao tu lakini lugha ya haijui, taarifa hizo kutokana na kucheza dhidi ya Napoli ambayo Rais wao Aurelio De Laurentiis alikuwa anamuhitaji Klopp kwa muda mrefu hazina mashiko.
Jurgen Klopp alifika mbali zaidi na kueleza kuwa wanaodhani anaweza akaondoka haoni kama nafasi hiyo ipo kwani bado ana kandarasi ya miaka mitatu na nusu, hivyo ametoa kauli inayoashiria kuwa hakuna timu itakayokuwa inamvumilia kwa miaka yote mitatu na nusu amalize mkataba na Liverpool ndio imchukue.
““Bado nina kandarasi ya miaka mitatu na nusu hapa sina uhakika kama kuna timu itanihitaji baada ya mkataba huo,”alisema Jurgen Klopp Miaka mitano iliyopita Jurgen Klopp akiwa Ujerumani katika timu ya Borussia Dortmund aliwahi kuhitajika kwenda kuwa kocha mkuu wa kikosi cha Napoli zaidi ya mara moja ila aliipiga chini ofa hiyo na kwena kwa majogoo wa jiji la London