Zlatan atupa dongo wa Cristiano Ronaldo
Licha ya kucheza kwa mafanikio makubwa katika klabu bora mbalimbali barani Ulaya, Zlatan Ibrahimovic hakuwahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Akihojiwa na kituo cha Fox Sports hivi karibuni kuhusu ushindi wa tuzo ya Ballon d’Or alioupata kiungo wa Real Madrid Luka Modric, nyota huyo wa timu ya La Galaxy ya Marekani, alitoa jibu ambalo liliwashangaza wengi
Mwandishi : “ Maoni yako ni yapi kuhusu Luka Modric kushinda Ballon d’Or ? “
Zlatan : “ Sasa tunaweza kuona kwamba Messi katika Ballon d’Or alikuwa anashindana na Florentino Perez, sio Cristiano “
Zlatan amedai kuwa Florentino Perez ambaye ni rais wa Real Madrid ana ushawishi mkubwa katika tuzo hiyo.