STERLING KAWAAMBIA POLISI KUWA ALITUKANWA NA KUBAGULIWA
Wakati klabu ya soka ya Chelsea chini ya uongozi wake ikiendelea na uchunguzi kuhusiana ni mashabiki gani ambao wamemtolea lugha ya kibaguzi nyota wa Manchester City Raheem Sterling wakati wa mchezo dhidi yao katika uwanja wa Stamford Bridge, Raheem Sterling ashitaki Polisi.
Raheem Sterling uchunguzi huo ukiendelea ni kweli ameamua kukiri na kuthibitisha polisi kuwa, mashabiki wa Chelsea walimbagua wakati anakwenda kuokota mpira wa kona wakati wa mchezo dhidi yao uliyomalizika kwa Manchester City kuvunja rekodi yao ya kucheza michezo 21 ya Ligi Kuu Uingereza bila kupoteza.
Sterling alihojiwa na Polisi waliokuwa wamesafiri kumfuata ili kupata maelezo yake, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tuhuma hizo za ubaguzi wa rangi, Sterling alifika mbali zaidi kuwa ni kweli alisikia lugha za kibaguzi na matusi dhidi yake ambayo yanaashiria ubaguzi wakati akiokota mpira wa kwenda kupiga kona.
Kuna hatari kubwa mashabiki wa Chelsea waliokuwa wametenda kosa hilo kama wakithibitika, wanaweza kukumbana na rungu la kufungiwa kutoingia uwanjani maisha, pamoja na kuwa vitendo vya kibaguzi vimeshamiri kwa baadhi ya nchi Ulaya lakini FIFA na vyama vya soka wanachama vimekuwa vikipiga vita vitendo hivyo kwa kutoa adhabu kali kwa wale watakaobainika kutenda kosa hilo.