Cristiano Ronaldo amkaribisha Messi Italia.
Ligi kuu nchini Hispania La Liga tangu mwaka 2009 ilibarikiwa kuwa na wachezaji nyota wawili wakali duniani, Cristiano Ronaldo akicheza Real Madrid na Lionel Messi akiwa Barcelona.
Baada ya miaka tisa, Cristiano Ronaldo aliamua kuondoka Hispania, kwa dau la pauni milioni 88 majira ya kiangazi mwaka huu akatua Juventus nchini Italia.
Cristiano Ronaldo ambaye ameshika hatamu katika ligi ya Italia, amesema kuwa hajai-miss Real Madrid au mpinzani wake Lionel Messi.
Lakini Ronaldo amemtaka mpinzani wake Lionel Messi ajiunge nae nchini Italia kabla ya hajamaliza maisha yake ya soka.
“ Hapana, labda yeye( Messi) ndio ameni-miss mimi “ Ronaldo ameliambia gazeti la Italia Gazzetta dello Sport.
“Nilicheza England, Spain, Italy, Portugal, katika timu ya taifa , wakati yeye akiwa bado yupo Spain.
“Labda yeye ananihitaji mimi zaidi. Kwangu mimi, maisha ni changamoto , ninazipenda na ninapenda kuwafanya watu wafurahi “
“Ningependa siku moja aje Italy “
“ Kama mimi, kubali changamoto . Hata hivyo, kama ana furaha hapo, ninaheshimu, ni mchezaji mzuri , ni mtu mzuri , lakini sija-miss chochote. Haya ni maisha yangu mapya na ninafurahi.