MAKAMBO ANAIFUNGA HAT-TRICK TP MAZEMBE AJE AISHINDWE NDANDA
Mwalimu Mwinyi Zahera wa Yanga baada ya ushindi wa mabao 2-1 wa Yanga dhidi ya Biashara United alipata fursa ya kuzungumzia mchezo huo ambao ulianza kwa wao kupoteza hadi dakika ya 70 Abdallah Shaibu alipoisawazishia bao timu hiyo na dakika ya 80 Makambo kufunga la ushindi.
Mwinyi Zahera amekiri kuwa wakati wa mapumziko timu yake ikiwa nyuma aliwatoa presha wachezaji wake kwa kuwaambia mnakumbuka wiki iliyopita kipindi cha kwanza Prisons walikuwa wanaongoza lakini walifanikiwa kupindua matokeo na kuondoka na alama tatu jijini Mbeya.
Kuhusu Makambo kocha Zahera anasema mchezaji huyo labda anajisahau tu lakini anamjua vizuri, hivyo ikitokea akafanya vibaya basi ujue ni kutokana na kujisahau kwake tu na kujiachia mwili wake ukanenepa, Zahera amekiri Makambo kuwa na uwezo mkubwa kiasi cha kuwahi kuisumbua hata TP Mazembe wakati akiichezea FC Lupopo.
“Hakuna siri yoyote leo tulijitaharisha kama tulivyojitaharisha katika mechi yoyote, Makambo mimi namjua toka yupo Congo anacheza na Mazembe anawafunga matatu akiwa na Lupopo sasa itakuwa hapa anacheza na Ndanda ashindwe kufunga goli kama anafanya vibaya itakuwa yeye mwenyewe anakula ugali kila siku ananenepa” alisema Mwinyi Zahera
Matokeo hayo yanawafanya Yanga wazidi kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 41 baada ya kucheza michezo 15, Azam FC ikiwafuatia kwa wakiwa na alama 39 na Simba nafasi ya tatu wakiwa na alama 27 na viporo vitatu.