COASTAL UNION IMESHINDWA KUPATA ALAMA TATU VS MBEYA CITY, ALIKIBA AKICHEZA KWA DAKIKA 64.
Mchezo wa 15 wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Coastal Union waliocheza dhidi ya Mbeya City mjini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani, ulimalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu ya kufungana kwa bao 1-1 wakati kivutio kikubwa kikiwa ni msanii wa Bongofleva Alikiba kucheza mechi yake ya kwanza.
Alikiba mchezo huo alipata nafasi ya kucheza kwa dakika 64 pekee kabla ya kufanyiwa na mabadiliko na nafasi yake kuchukuliwa na Deo Anthony ila akiondoka uwanjani akiwa ameacha Coastal Union ikiwa 1-1 baada ya kusababisha kona iliyozaa bao lililofungwa na Ayoub Lyanga mapema mwanzoni mwa mchezo dakika ya 5.
Sare hiyo inawafanya Coastal Union kugawana alama moja moja na wageni wao Mbeya City kutoka jijini Mbeya, kwa asilimia 59 Coastal Union waliutawala mchezo na kufika langoni mwa Mbeya City mara nyingi sema goli la kujifunga kwa Bakari ndio limewanyima kuvuna alama tatu katika mchezo huo ila mchezo ulitawaliwa na madhambi 40, Coastal wakicheza mara 18 wakati Mbeya City mara 22.