Mo Salah ampa tuzo Milner
Kiungo mahiri wa Liverpool aliyedumu na timu hiyokwa misimu mitano James Milner leo baada ya mchezodhidi ya AFC Bournemouth alipewa tuzo na mchezajimwenzake raia wa Misri Mohamed Salah aliamua kumpazawadi ya tuzo yake ya mchezaji bora wa mechi kamaishara ya kuheshimu Milner kucheza mchezo wake wa500 Ligi Kuu Uingereza.
Baada ya mchezo huo Mohammed Salah katikamahojiano na waandishi wa habari alienda moja kwamoja Milner na kumkabidhi tuzo hiyo huku akimpongezakwa kufikisha jumla ya michezo 500 ya Ligi KuuUingereza ambayo amechezaji akiwa na timu tofautitofauti ikiwemo Liverpool.
Mchezo ulimalizika kwa Liverpool kupata alama tatu namabao 4-0 kati ya hayo matatu yamefungwa hat-trick naMohammed Salah aliyeamua kutoa tuzo yake yamchezaji bora wa mechi kwa James Milner ambayeamekuwa akiamini anastahili makubwa kwani kuchezamechi 500 Ligi Kuu Uingereza sio kitu kidogo.