MENDES AMETOA TAMKO KWA JOSE MOURINHO
Wakala wa kocha wa Manchester United Jose Mourinho wakala wake akijulikana kwa jina la Jorge Mendes ameamua kuweka wazi msimamo wa mteja wake na klabu yake ambapo klabu imekuwa ikidaiwa kutaka kumfuta kazi ila Mendes ameweka wazi msimamo wa Mourinho.
Mendes ameweka wazi kuwa mteja wake ana furaha kuendelea kuifundisha Manchester United tofauti na watu wanavyosema na Manchester United wanafuraha na Jose Mourinho, hivyo wanaozusha kuwa atafutwa kazi aanze kuwaza mawazo.
“Kuna tetesi kuwa Jose Mourinho anaondoka Manchester United ana mkataba mrefu na Manchester United kwa ajili ya kutengeneza kikosi imara cha ushindi” alisema Jorge Mendes katika taarifa rasmi aliyoamua kuitoa na kuisambazo
Manchester United ambao walimaliza nafasi ya pili msimu uliopita, sasa hivi wanaendelea kuwa nafasi mbaya nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Uingereza na wana alama 23 wakicheza michezo 15, ushindi michezo 6, sare mitano na wapoteza michezo minne.
Tukukumbushe wakala Jorge Mendes amekuwa ni miongoni mwa watu maarufu wanaosimamia mashabiki na makocha wa soka, Mendes pia ndio wakala wa staa wa Juventus Cristiano Ronaldo, lakini amewahi kufanya kazi pia na watu mbalimbali kama Carlos Tevez.