Joe Gomez sana anahitaji siku 42 kurejea uwanjani
Mchezaji wa Liverpool Joe Gomez aliyeumia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Uingereza kati ya Liverpool dhidi ya Burnley, Joe Gomez tayari amefanyiwa uchunguzi na kuruhusiwa kuondoka hospitalini akiwa na magongo hiyo ni baada ya kuumia kifundo cha mguu wakati wa mchezo dhidi ya Burnley.
Joe Gomez sasa baada ya uchunguzi wakina na kupatiwa matibabu atahitaji kuwa nje ya uwanja kabla ya kuanza mazoezi mepesi kwa siku 42 ambazo ni sawa na wiki sita, hivyo ni wazi mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kumaliza mwaka 2018 taarifa zikithibitishwa na Liverpool.
Hata hivyo mchezo uliomuweka Joe Gomez nje ya uwanja ulimalizika kwa Liverpool kupata ushindi wa mabao 3-1 na kuwafanya wakusanye jumla ya alama 39 katika Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2018/2019 wakiwa nafasi ya pili nyuma ya Manchester City wanaoongoza Ligi kwa kuwa na alama 41.