Scholes kahoji wanaomuhitaji zidane ndani ya Manchester United
Kwa miezi kadhaa kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekuwa akihusishwa kuwa yupo mbioni kutimuliwa kazi katika klabu ya Manchester United baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo na nafasi yake ichukuliwe na kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane.
Kufuatia taarifa hizo ambazo hazijathibitika kuzidi kusambaa katika mitandao ya kijamii, mchambuzi wa soka wa BT Sport ambaye amewahi kuichezea Manchester United kwa miaka kadhaa Paul Scholes amehoji wanaomini Zidane anaweza kumrithi Mourinho kuwa wanahisi ataisadia Mancheset United.
Mourinho amekuwa katika presha kubwa kwa sasa ndani ya klabu hiyo kutokana na kutofanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu na kujikuta wapo nafasi ya nane wakiwa na tofauti ya alama 18 dhidi ya Manchester wanaoongoza Ligi Kuwa na alama 41, hivyo ni wazi Mourinho amekalia kuti kavu katika kazi yake.
Scholes amehoji wanaomtaka Zidane wanahisi ana uzoefu wa kutosha kumritho Mourinho
“Zidane ni mtu sahihi? Alienda Real Madrid katika kundi ambalo tayari lilikuwa limeshawatengeneza washindi hii kwa ujumla ni kazi ngumu atatakiwa atengeneze hali ya kujiamini kwa wachezaji ambao wamekuwa hawachezi vizuri, alienda Real Madrid ikiwa ni timu ambayo tayari inaundwa na wachezaji wakubwa” alisema Scholes Tukukumbushe tu Zidane aliondoka Real Madrid mwezi Mei akiwa ameisaidia timu hiyo kushinda mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na LaLiga lakini baada ya kukaa nje ya uongozi wa soka kwa miezi sita, Zidane ameripotiwa kuwa yupo tayari kurudi kuendelea na ajira ya kufundisha soka.