Simba SC sasa kucheza dhidi ya Hassan Kessy Ligi ya Mabingwa
Shirikisho la soka Afrika CAF limepanga ratiba ya michezo ya pili ya michuano ya klabu Bingwa Afrika msimu wa 2018/2019, baada ya Simba SC kuwatoa Mbabane Swallows ya Swaziland kwa jumla ya mabao 8-1 katika mzunguuko wa kwanza sasa wamepangwa kucheza Zambia.
Simba SC baada ya kupata matokeo hayo na kuvuka mzunguko wa kwanza kwa kishindo sasa CAF wamewapanga kucheza mzunguko wa pili na timu ya Nkana ya Zambia hiyo ikiwa muendelezo ya michezo ya kuwania kuingia hatua ya makundi.
Kutokana na ratiba hiyo Simba SC sasa watakuwa wanacheza dhidi ya mchezaji wao wa zamani Hassan Kessy ambaye kwa sasa anaitumikia timu hiyo ya Nkana ya Zambia, mchezo wa kwanza Simba itacheza dhidi ya Nkana nyumbani.
Simba wanapata nafasi hiyo baada ya Nkana kuwafunga UD Songo 1-0 na ukilinganisha mchezo wa kwanza ugenini walishinda 2-1, basi wanafuzu kwa jumla ya ushindi wa mbao 3-1, tukukumbushe tu Kessy aliwahi kucheza Simba SC baadae Yanga SC na kuamua kutimkia Nkana ya Zambia