Fainali ya Copa Libertadores imepelekwa Ulaya, Mashabiki waifuata
Klabu ya Boca Junior imewasili Hispania katika jiji la Madrid kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa marudiano wa fainali ya Copa Libertadores dhidi ya River Plate ambapo mchezo huo unaambiwa kuwa utachezwa katika uwanja wa Real Madrid ujilikanao kama Santiago Bernabeu kukiwa na maafisa usalama zaidi ya 2500.
Mchezo wa River Plate dhidi ya Bocca Junior uliahirishwa kutokana na vurugu za mashabiki zilizokuwa zimetokea na maamuzi yakafanyika kuwa mchezo huo ukachezwe nje ya Argentina ndipo uongozi wakaona ni vyema kwenda kuchezwa Hispania katika mji wa Madrid uwanja wa Santiago Bernabeu.
Hata hivyo taarifa zinaeleza na kusema kuwa mchezo kati ya Bocaa Junior na River Plate unaochezwa katika bara la Ulaya ndio unatajwa kuwa mchezo wenye hatari zaidi Ulaya na inatajwa kuwa kuna uwezekano wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kuhudhuria mchezo huo kama mashabiki wa kawaida kitu ambacho kimemfanya Rais wa Real Madrid kutamani kutaka wachezaji hao wakae pamoja kama sehemu ya kusherehekea miaka 10 yao ya utawala katika soka hiyo ni kwa mujibu wa Clipfooty.
Mchezo wa kwanza wa timu hizo ulichezwa katika uwanja wa Bocca Junior na kumalizika kwa sare ya 2-2 lakini mchezo wa marudiano uliyokuwa umepangwa kuchezwa Buenos Aires ulishindwa kuchezwa baada ya mashabiki wa River Plate kuwashambulia wachezaji wa Bocca Junior Novemba 24 na sasa umeamuliwa kuchezwa Madrid Jumapili huku mashabiki wa vilabu hivyo wapatao 10000 wanatajwa kusafiri kuifuata mechi hiyo.