Man U wamenusurika nyumbani dhidi ya Arsenal
Manchester United wamecheza mchezo wao wa 15 wa Ligi Kuu Uingereza wakiwa katika uwanja wao wa Old Trafford na kujikutana wakiambulia sare ya kufungana mabo 2-2, mabao ya , Manchester United yakifungwa na Anthony Martial dakika ya 30 na Jesse Lingard dakika ya 69 wakati ya Arsenal yamefungwa na Mustafi dakika ya 26 na Alexandre Lacazette dakika ya 68.
Sare hiyo inaiondoa Arsenal TOP 4 na kuisogeza hadi nafasi ya tano wakiwa na alama 31 wakati Manchester United nao wanashuka hadi nafasi ya nane kwa kufikisha jumla ya alama 23, ila Arsenal wanaondoka Old Trafford wakiwa wamefanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 56 kwa 44.
Hata hivyo sare hiyo inawafanya Arsenal waendelee na rekodi yao ya miaka 12 ya kutoifunga Manchester United katika uwanja wa Old Trafford, mara ya mwisho Arsenal kufanya hivyo ilikuwa mwaka September 2006 hivyo bado wanaendelea kusubiri kuivunja rekodi hiyo, Manchester United na Arsenal hii ni mara ya 228 kuwahi kucheza na Manchester United wameshinda mara 98 wamepoteza mara 82 na sare 48.