Sarri kafunguka Hazard kapewa mkataba kazi kwake
Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri amefichua siri kuwa uongozi wa Chelsea tayari umemuweka mkataba mezani mbelgiji Eden Hazard sasa jukumu litakuwa lake sasa kuusaini au kutousaini mkataba huo.
Mkataba mpya wa Hazard na Chelsea utamfanya awe mchezaji pekee katika historia ya timu hiyo kulipwa mshahara mkubwa ila Hazard bado hajamua kusaini mkataba huo akisubiri msimamo wa Real Madrid dhidi yake ambao walikuwa wakimuhitaji kwa muda mrefu sasa.
Hazard mkataba wake na Chelsea unamalizika mwisho wa msimu huu na anahusishwa kuwa mbioni kujiunga na Real Madrid licha ya mwenyewe kuweka wazi kuwa ana mpango wa kwenda kucheza soka Hispania, kama Hazard akisaini mkataba mpya Chelsea atakuwa analipwa mshahara wa pauni 300000 kwa wiki.
Kocha Maurizio Sarri kuelekea mchezo wao na Wolves leo amesema anamuhitaji Hazard ila itakuwa ni uamuzi wake kuamua kuendelea kubaki na Chelsea au kuondoka katika timu ila mazungumzo ya kumshawisho nyota huyo asalia Stamford Bridge yamekuwa yakifanyika kila wiki.
“Namtaka sasa Hazard abaki Chelsea lakini nataka abaki kama mwenyewe atataka kubaki naelewa vizuri kuwa kuna mazungumzo yanaendelea kila wiki kati ya klabu na mameneja wa Hazard” alisema Maurizio Sarri