Nikola wa Leopards ahusishwa na Free State Stars
Kocha wa AFC Leopards Nikola Kavazovic amehusishwa na Klabu ya Afrika Kusini, Free State Stars.
Raia huyo wa Serbia yupo kwao nyumbani baada ya kuondoka nchini Kenya siku ya Jumamosi. Kulingana na taarifa kutoka Leopards, alirejea kwao kuhudhuria jambo la dharura.
Habari kutoka Afrika Kusini yasema kuwa kocha huyo ni miongoni mwa makocha ambao wamehusishwa na Klabu ya Free State Stars ambayo inasaka kocha baada ya kuondoka kwa Luc Eymael ambaye vile vile ni kocha wa kitambo wa timu ya Chui.
Iwapo ataondoka Leopards, litakuwa pigo kubwa ikizingatiwa kuwa msimu wa 2018-19 unaanza wikendi ijayo.
Nikola alijiunga na Leopards mwezi November kutoka klabu ya Botswana, Township Rollers.