Jose Mourinho awageukia MU TV
Manchester United kesho watakuwa na mchezo wa kukata na shoka katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford dhidi ya Arsenal ukiwa ni mchezo wa muendelezo wa michezo ya Ligi Kuu Uingereza msimu huu.
Kikosi cha Manchester United bado kinatajwa kuwa kitakuwa na presha kubwa kuikabili Arsenal wakiwa katika uwanja wao, kwani Manchester United wamekuwa na mwanzo mbaya msimu huu kitu ambacho kinapelekea presha kubwa kwa kikosi hicho kucheza nyumbani.
Kuelekea mchezo huo kocha wa Manchester United Jose Mourinho aliongea na waandishi wa habari ikiwa ni kawaida kufanya hivyo siku moja kabla ya mchezo husika, Mourinho aligoma kujibu swali la MU TV yaani TV ya klabu yake kutokana na kutotaka kuweka wazi baadhi ya taarifa na kuwaambia kuwa maswali wanayouliza walipaswa kumuuliza Arsenal TV.
“Sitaki kukujibu wewe nataka mtu wa Arsenal TV ndio aulize swali kama hilo nimjibu lakini hawataki, kwa hiyo kwa nini nikujibu wewe” alisema Mourinho kauli ambayo imegoma kuweka wazi safu yake ya ulinzi atakayoitumia kesho licha ya kuwa amekuwa na changamoto sana hivyo kujibu swali hilo anaona kama ni kutoa mbinu zake kwa wapinzani.