Stand United wametaja walipojikwaa Chamazi
Stand United wamekosa bahati katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wao Azam FC kutokana na kujikuta wanapoteza pamoja na kupata bao la uongozi mapema na Azam FC kukaa na presha juu kwamba wanaweza kupoteza mchezo huo.
Mchezo huo ukichezwa usiku wa leo katika uwanja wa Chamazi, Stand United wamebugizwa kipigo cha mabao 3-1, shukrani za dhati Azam FC wanapeleka kwa Yahaya Zayd aliyeingia na kuja kubadili taswira nzima ya mchezo huo na kujikutana Azam FC wanasalia na alama tatu nyumbani na kuendelea na nafasi yao ya pili wakiwa na alama 36 na Stand nafasi ya 15 wakiwa na alama 14 na wamecheza michezo 15 wakiizidi Azam FC mchezo mmoja.
Yahaya Zayd anaingia akitokea benchi na kuwa msaada wa kupatikana kwa mabao yote matatu la kwanza akitoa usaidizi kwa Enock Atta na mawili akifunga kwa penati na njia ya kawaida, wakati Stand wao waliishia bao moja lililofungwa na Hafidh Musa dakika ya 53.
Baada ya mchezo Jacob Masawe wa Stand United alieleza wamekwama wapi na kujikuta mchezo ukibadilika na wao kupoteza “Tunashukuru Mungu tulivyoingia kipindi cha pili tukaweza kupata goli nadhani baada ya kupata goli tuka tumeridhika na kutengeneza makosa mengi ambayo Azam wameyatumia mimi namshukuru Mungu”alisema Masawe