Kahata kukosa Mechi didhi ya Nyasa
Kiungo wa Gor Mahia, Francis Kahata kwa mara nyingine atakosa mechi ya marudiano kwenye Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya timu ya Malawi, Nyasa Bullets itakayochezwa siku ya Jumatano huko Malawi.
Kahata alikosa mechi ya kwanza kwani yupo kwenye harakati ya kujiunga na kilabu ya Algeria CS Constantine.
Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amethibitisha kuwa Kahata atakosa mechi hiyo kwa kuwa kuchezea Gor kwenye ligi ya Mwabingwa huenda ikamnyima nafasi ya kuelekea Algeria.
“Kahata atakosa mechi ya Nyasa Bullets kwani akicheza, klabu hiyo itagoma kumsaini. Nina imani wachezaji watakaocheza wataandikisha matokeo mema,” alisema Rachier.
Wachezaji wengine watakao kosa mechi hiyo ni pamoja na mshambulizi Jacques Tuyisenge na Kiungo Kenneth Muguna ambao wanauguza majeraha.