Wambura arejea TFF
Baada ya miezi tisa kupita toka kamati ya maadili itangaze kumfungia maisha kujihusisha na soka kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) ndugu Michael Richard Wambura, leo ameibuka na mapya kuhusiana na uamuzi huo.
Wambura akiambatana na mwanasheria wake Emmanuel Muga leo amewasilisha hati ya Mahakama Kuu ya Kupinga kufungiwa kwake maisha kujihusisha na soka na kudai kamati ya maadili ya TFF ilikiuka baadhi ya kanuni wakati wa kumfungia kwake hivyo, Mahakama imetengua maamuzi ya kamati ya maadili ya kumfungia Wambura.
Tukukumbushe tu Michael Richard Wambura alifungiwa maisha kujihusisha na soka Machi 15 2018 kutokana na kutuhumiwa kwa makosa matatu ambapo moja ni kupokea pesa za TFF isivyo halali, kugushi nyaraka na kosa la tatu kushusha hadi ya shirikisho hilo.