Hatimae PSG wamesimamishwa LIGUE 1
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Ufaransa klabu ya Paris Saint Germain leo imekutana na bahati mbaya na kuvunjwa kwa rekodi yao ya kushinda michezo 15 mfululizo baada ya Bordeaux kufanikiwa kuondoka na point.
Mchezo wa Ligi Kuu Ufaransa kati ya wenyeji Bordeaux dhidi ya PSG leo umeandika historia mpya Ligi Kuu Ufaransa kufuatia kuisimamisha PSG iliyokuwa inashinda kila mchezo wa Ligue 1 msimu huu, imejikuta ikipata sare ya kwanza kwa kufungana mabao 2-2.
Baada ya Neymar kufunga bao la kwanza dakika ya 34 na Jimmy Briand dakika ya 53 akaisawazishia Bordeaux, Kylian Mbappe alirudi wavuni dakika ya 66 na kufunga bao la pili lililokuwa limeleta imani kuwa PSG wataondoka na alama tatu ila dakika sita kabla ya mchezo kumalizika Bordeaux kupitia kwa Andreas Cornelius akafunga bao la kusawazisha na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2 na kugawana moja kila timu.
Bordeaux ndio inakuwa timu ya kwanza Ligue 1 msimu huu kuondoka na alama walau moja dhidi ya PSG, ambao walikuwa wamecheza michezo 14 na kushinda yote kabla ya mchezo wao wa 15 kusimamishwa na Bordeaux, PSG wanaendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 43 wakifuatiwa na Montpeller wenye alama 29 huku Bordeaux licha ya sare hiyo wameshuka hadi nafasi ya 11 wakiwa na alama 18.