Tyson Fury ameamua kutoa msaada wa Tsh Bilioni 23
Mwanamasumbwi wa Uingereza Tyson Fury baada ya kuvunjika kwa rekodi yake ya kupata ushindi katika mapambano yote, pambano lake dhidi ya Wilder lilimalizika kwa kutoka droo kutokana na kufanikiwa kumaliza kwa round zote 12 wakiwa wametoshana nguvu.
Fury ambaye kabla ya pambano na Wilder alicheza mapambano mawili ya kupasha mwili moto, alikuwa nje ya ulingo kwa miaka miwili na sasa kufuatia droo ya pambano dhidi ya Wilder ametangaza kuwa anatoa msaada wa pauni milioni 8 ambazo ni sawa na Tsh Bilioni 23 kwa watu wasiojiweza na waliokuwa hawana makazi.
Tukukumbushe licha ya droo kutangazwa mashabiki walilalamika kuwa Fury alikuwa anatakiwa kutangazwa mshindi kwani amefanikiwa kumiliki pambano kwa round zote 12, ukilinganisha na Wilder ambaye wanadai alielemewa zaidi katika round zote.
Pambano hilo mgawanyo wa alama kwa mabondia hao ulikuwa hivi 115-111 kwa Wilder na 114-110 kwa Fury ambapo ni sawa na 113 kwa 113 kwa kila bondia hivyo hakuna aliyebahati kuondoka na ushindi licha ya mabondia wote kuwa na rekodi ya kutopigwa katika mapambano yao.