KOCHA WA LIVERPOOL JURGEN KLOPP AMEOMBA RADHI
Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ametangaza kuomba radhi kwa kitendo chake alichokionesha wakati akishangilia ushindi wa lala salama wa Liverpool dhidi ya Everton, mchezo ambao ulikuwa kivutio katika jiji la Liverpool kwa kuzikutanisha timu za mji mmoja.
Klopp ameomba radhi kufuatia kitendo chake cha kushangilia bao pekee la ushindi la Liverpool lililofungwa dakika za nyongeza na Divock Origi aliyeingia dakika ya 84 akitokea benchi kuchukua nafasi ya mbrazil Roberto Firmino, hivyo Klopp baada ya goli kuingia alishangilia umbali wa yard 40 kutoka eneo lake la ufundi kitu ambacho hakileti picha nzuri.
“Derby siku zote ni game ngumu zinakuwa lakini hii ilikuwa ina ugumu wa tofauti kwa miaka michache iliyopita, ninachoweza kusema katika hili sikuwa nimepanga kukimbia wala haikuwa katika mipango yangu sikuwa nimepanga kukimbiwa kwa Alison, nisingeweza kujizuia lakini ndio imetokea, kitu muhimu kinachoweza kutokea dakika ya 95 ila nawaheshimu sana Everton” alisema Klopp
Klopp kufuatia kitendo hicho amemuomba radhi kocha wa Everton Marco Silva na anaakiri kuwa hakufanya vizuri, ushindi wa bao 1-0 wa Liverpool sasa unawaweka nafasi ya pili ile ile walioyokuwa kabla ya mchezo kwa kufikisha alama 36 tofauti ya alama mbili na Manchester City wanaongoza Ligi kwa alama 38 Everton wakibaki nafasi ya 6 kwa kuwa na alama zao zile zile za awali 22.