Kocha wa Gor atua Kenya
Kocha Mpya wa Gor Mahia, Hassan Oktay ametua nchini na anatarajiwa kuchukua hatamu kwenye mabingwa hao wa Kenya.
Mkufunzi huyo mwenye asili ya Uturuki anatokea kwenye Kilabu ya Braintree nchini uingereza na anachukua nafasi ya Dylan Kerr ambaye aligura na kuelekea Afrika Kusini.
Oktay alihudhuria mechi Kati ya Gor Mahia na Kariobangi Sharks siku ya jumapili, mechi ambayo Sharks iliwachabanga miamba hao bao moja kwa yai.
Oktay na kikosi chake wataelekea nchini Malawi siku ya Jumatatu kwa mechi ya marudiano didhi ya timu ya Nyasa Bullets kwenye Kombe la CAF.
Oktay atasaidiwa na Zedekiah Otieno ambaye amekuwa kocha msimamizi tangu alipo ondoka Kerr.