Mohomed Hussein amesema dakika 45 wamecheza Dar na dakika 45 za pili watacheza Swaziland
Ushindi wa mabao 4-1 Simba SC ikirejea kwa mara ya kwanza katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya miaka mitano kupita, umepokelewa kwa furaha kwa upande wa mashabiki na hata viongozi.
Baada ya ushindi huo nahodha msaidizi wa Simba SC Mohamed Hussein aliongea na Azam TV na kueleza kuwa licha ya ushindi wa mabao mengi walioupata hawawapi fursa ya kujisahau na wao wanauchukulia mchezo huu wa awali ni kama dakika 45 kwanza na mardiano watacheza Mbabane ndio dakika 45 za pili,
“Ni kweli tuliingia kwamba wapinzani wasiweze kupata goli lakini katika game lolote linaweza kutokea kikubwa tumepata idadi kubwa ya magoli na tumemaliza dakika 45 za kwanza Dar na tunaenda Swaziland kucheza dakika 45 za pili tutahakikisha kuwa tunaenda kuzuia au kufunga na kusonga mbele” alisema nahodha msaidizi wa Simba SC Mohamed Hussein
Tukukumbushe tu baada ya matokeo hayo Simba SC watalazimika kwenda Mbabane nchini Swaziland kucheza mchezo wa marudiano huku wakiwa wanahitaji sare ya aina yoyote au afungwe chini ya mabao matatu katika mchezo wa Marudiano Decemba 4 au 5, 2018.