Mnyama arejea kwa kishindo klabu bingwa Afrika
Baada ya miaka mingi kupita Simba SC wanarudi katika michuano ya klabu bingwa Afrika.
Wamerudi kwa kishindo kizito. Leo katika dimba la uwanja wa Taifa Dar es salaam Simba imewachinja Mbabane Swallows kutoka Swaziland goli 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi ya awali klabu bingwa Afrika
Magoli ya Simba SC yamewekwa kimiani na nahodha John Bocco ambaye alifunga mawili, dakika ya 7 na dakika ya 32 ambalo alifungwa kwa mkwaju wa penati. Meddie Kagere aliendeleza moto wake katika msimu wake wa kwanza Simba akifunga goli dakika ya 84, akitumia vyema makosa ya kipa Mbabane Swallows aliyeteleza baada ya kurudishiwa mpira na mchezaji mwenzake.
Clatous Chama ndiye mchezaji aliyeng’ara zaidi katika mechi hii, dakika ya 90 alifunga goli kwa kupiga shuti kali ambalo lilimuacha kipa wa Mbabane akihangaika chinii.
Goli la wageni lilifungwa dakika ya 24 na Nzambe kwa shuti kali
Baada ya ushindi huo, Simba itarudiana na timu hiyo nchini Swaziland jumatano ijayo Disemba 5 na mshindi kati ya timu hiyo katika raundi hii ya awali, atakuwa amefuzu raundi ya kwanza ya michuano hii.