MASHABIKI WASIHOJI TENA TFF, IMEWEKA MAMBO SAWA
Kwa siku kadhaa sasa kumekuwa na malalamiko kuwa mchezo wa JKT Tanzania dhidi ya Yanga ambao unaripotiwa kuwa JKT Tanzania atakuwa mwenyeji utachezwa uwanja wa Taifa na sio Mkwakwani tena kama ilivyokuwa mchezo wa Simba na JKT Tanzania.
Tukukumbushe tu JKT Tanzania waliomba kutumia uwanja wa Mkwakwani Tanga kama uwanja wao wa nyumbani kwa michezo ya Simba na Yanga na hawautaki Taifa kutokana na uwanja huo kuwapendelea sana vilabu hivyo kutokana na kuuzoea vizuri.
Hivyo shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeweka wazi kuwa mashabiki wasiwe na hofu mchezo wa JKT Tanzania na Yanga unaochezwa uwanja wa Taifa ni Yanga ndio mwenyeji hakuna mabadili ila mchezo wa marudiano wa timu hizo utachezwa Mkwakwani kama kawaida Februari 9 2019 kama ambavyo JKT waliomba kutumia uwanja huo kama uwanja wao wa nyumbani.