Hemed Morocco asajili wachezaji wanne wa kimataifa kwa mpigo
Baada ya klabu ya Singida United kuwapoteza wachezaji wake kadhaa wakiwemo Miraji Adam aliyejiunga na Coastal Union ya Tanga jana na Salum Chuku aliyejiunga na KMC ya Kinondoni jana, leo uongozi wa klabu hiyo umetangaza kufanya usajili wa kuimarisha timu yao.
Singida United inayofundishwa na kocha wao Hemed Morocco imeripotiwa kuwasajili wachezaji wanne kwa mpigo wa kimataifa wa Zambia wanaocheza timu ya vijana ya Taifa ya wenye umri chini ya miaka 23.
Wachezaji hao wa kigeni ambao wanatajwa kuwa ndio wamekuja kuimarisha timu hiyo ambayo inapitia kipindi kigumu kwa sasa kiuchumi ni pamioa na Chikwangala, Mwale, Jordan Daka na G Mwale.
Singida kwa sasa katika msimamo wa Ligi ipo nafasi 9 ikicheza michezo 14 ikiwa na alama 18 tofauti na msimu uliopita wakati kama huu ilikuwa ndani ya TOP 5.