Mke akanusha kiaina mumewe kuondoka Liverpool Januari
Tunaelekea dirisha dogo la usajili barani Ulaya na tayari tumesikia wachezaji nyota wakihusishwa kutoka klabu moja kwenda nyingine kwa sababu tofauti tofauti wengine maslahi na wengine mapenzi tu na mahali familia yake ingependa kuishi.
Baada ya baadhi ya mitandao kuripoti kuwa kiungo wa Brazil anayeitumikia Liverpool Fabinho anaweza akarudi kucheza soka Ufaransa safari hii akiwa na klabu tofauti ya Paris Saint Germain, taarifa hizo zimekanushwa na mkewe.
Ripoti nchini Ufaransa zinadai kuwa kocha wa PSG Thomas Tuchel amemuweka katika mahesabu yake Fabinho kwa ajili ya kumsajili mwezi Januari, tetesi hizo zikipewa nguvu na kauli ya Tuchel wiki kadhaa nyuma kuwa Fabinho ni moja kati ya viungo wakabaji bora Ulaya kwa sasa.
Tweet ya mke wa mchezaji huyo anayefahamika na wengi kwa jina la Rebecca Tavres inaashiria kuwa Fabinho hawezi kuondoka Liverpool “Pale ninaposoma baadhi ya habari batili twitter”
Tukukumbushe tu Fabinho mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Liverpool mwezi Mei mwaka huu 2018 akitokea AS Monaco ya Ufaransa kwa uhamisho unaotajwa kufikia pound milioni 43 licha ya kuwa amepata kuanza mechi tano tu toka ajiunge na Liverpool.