Mtibwa Sugar waanza kwa kishindo michuano ya kimataifa
Kikosi cha Mtibwa Sugar kimefanikiwa kuanza vizuri michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kushinda kwa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huo umeweka rekodi mpya kwa Mtibwa ya kufunga ‘Hat-trick’ ya Jaffary Kibaya ambaye amefanikiwa kutumia nafasi ambazo walizitengeneza Mtibwa leo.
Jaffary alifunga bao la kwanza dakika ya 13, la pili dakika ya 36 na dakika ya 58 kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa na walinzi wa Dynamo kwenye eneo la hatari.
Mabao hayo matatu yamemfanya kibaya kufikia rekodi ya Joseph kaniki kama mfungaji bora wa muda wa mtibwa kwenye mashindano ya Afrika
Katika dakika za lala salama mchezaji Raphael Khamis alifunga bao la 4 na la mwisho ambalo limewafanya Mtibwa Sugar kuibuka na pointi tatu na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani hivyo ili waweze kusonga mbele wanatakiwa kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa Disemba 5.