Singida United yaendelea kuwabomolewa
Klabu ya Singida United ya Singida licha ya kupanda Ligi Kuu kwa kasi na kuanza kuvisumbua vilabu vikongwe kama Simba na Yanga kupata matokeo chanya dhidi yake, msimu huu imeonekana ikiyumba na kutolewa katika orodha ya vilabu vitakavyoleta ushindani katika Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu.
Kukiwa bado wanajitafakari wanakosea wapi tofauti na msimu uliopita walivyokuwa wakisumbua, Singida imeondokewa na wachezaji wake wawili kwa mpigo na kuacha pengo, Singida leo katika dirisha dogo la usajili imempoteza beki wake Miraji Adam aliyejiunga na timu yake ya zamani ya Coastal Union kwa mkataba wa mieizi sita.
Hata hivyo pia imempoteza Salum Chuku aliyeamua kujiunga na klabu ya KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni, Salum Chuku amejiunga na KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida United, hata hivyo kinachoendelea kinahusishwa na mkurugenzi wao Festo Sanga kukiri kuwa klabu imeyumba kiuchumi.
Singida kwa sasa katika msimamo wa Ligi ipo nafasi 9 ikicheza michezo 14 ikiwa na alama 18 tofauti na msimu uliopita wakati kama huu ilikuwa ndani ya TOP 5.