Simba SC kuwavaa Waswaziland Jumatano
Klabu Bingwa ya soka Tanzania Bara Simba itashuka uwanja wa Taifa kupambana na mabingwa wa Swaziland Mbabane swallows hapo Jumatano saa 10 kamili jioni.
Akiongea na waandishi wa habari hii leo,Ofisa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema timu yao iko kambini kujifua na mchezo huo na wachezaji wako salama isipokuwa shomari Kapombe ambae yuko kwenye Matibabu baada ya kuumia kwenye mazoezi na timu ya Taifa huko Afrika ya kusini.
Manara amesema Mbabane ni timu nzuri, ni mabingwa wenzao na wanamatarijio kupata matokeo katika mchezo huo hivyo kuwasihi watanzania na mashabiki wa simba kufika uwanja wa taifa kuwatia nguvu wachezaji hao
Pia amesema “tunateswa na kauli ya Rais Magufuli ya kuwataka waweze kushinda katika mashindano ya kimataifa hivyo hawatawaangusha watanzania”
Mbabane swallows watawasili hii leo saa 7 usiku tayari kwa mchezo huo wa klabu bigwa Afrika raundi ya awali