Kocha wa Bandari aondoka na tuzo ligi ya Kenya
Kocha wa Timu ya Bandari Bernard ametuzwa kama kocha bora wa mwezi wa Agosti Katika Ligi ya Kenya.
Mwalala ambaye aliwahi kuichezea Timu za Yanga na Coastal Union kabla ya kuifunza Union kama naibu msaidizi aliiongoza Bandari kushinda mechi zake zote katika mwezi wa Agosti.
Bandari iliweza kuilaza timu za Posta Rangers, Gor Mahia, Tusker FC na Timu ya Mwalala ya Zamani, Nzoia Sugar.
Mwalala alikabidhiwa Nyara na hundi ya shillingi elfu sabini na tano za Kenya. Ni mara yake ya kwanza kushinda tuzo hili ambalo hudhaminiwa na kampuni ya bima ya Fidelity na kuendeshwa na Chama cha wanahabari wa spoti Kenya (SJAK).
Anakuwa kocha wa nane kushinda tuzo ili mwaka huu. Kocha wa Mathare Francis Kimanzi alishinda katika mwezi wa Februari naye Kocha wa Leopards Dennis Kitambi akalishinda mwezi wa Machi.
Mwezi wa nne Kocha wa Zoo Sammy Okoth alituzwa nalo tuzo la mwezi Mei likamwendea kocha wa Nakumatt Anthony Mwangi. Mwezi Juni kocha wa Gor Mahia Dylan Kerr alituzwa. Patrick Odhiambo wa Sony alitia kibindoni tuzo la mwezi Julai.