Hazard aendelea kuwaweka roho juu Chelsea
Siku zinahesabika kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa klabu mbalimbali Ulaya, hivyo sio jambo la ajabu sana kusikia mchezajiflani akitangazwa kuhusishwa kwenda katika timuFulani, kwa upande wa Chelsea wanaweza kupata pigokwa kuondokewa na mchezaji wao tegemeo raia wa Ubelgiji Eden Hazard.
Eden Hazard amerudia kauli yake ambayo inawaumizamashabiki wengi wa Chelsea kwa sasa kuwa anauwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo, Chelsea tayari wamemalizana na Ngolo Kante kwakumuongezea mkataba mrefu na sasa wanapambanakuhakikisha Hazard anasalia katika kikosi cha Maurizio Sarri.
“Kwa sasa nabakia Chelsea nina mkataba hadi mweziJuni mwakani kama sitaongeza mkataba basi kunauwezekano wa kuondoka lakini sioni nikiondoka Chelsea mwezi Januari, nisingependa kufanya hivyo kwa klabuna mashabiki lakini katika kipindi cha usajili cha majiraya joto naona uwezekano wa mimi kuondoka lakini piainawezekana nikamalizia soka Chelsea” alisema Hazard akihojiwa na Canal Plus
Hadi sasa Eden Hazard amedumu na Chelsea kwa miakasita toka alipojiunga na timu hiyo mwaka 2012 akitokeaklabu ya Lille ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wapound milioni 32, kwa miezi kadhaa sasa Hazard amekuwa akihusishwa kuhitajika na Real Madrid lichayay eye kukiri kuhitaji kwenda kucheza soka Hispania.