Gor Mahia yawazindua wachezaji wapya Wanane
Mabingwa wa Kenya imewazindua wazi wachezaji wanane wapya ikiwa imesalia majuma mawili kabla msimu mpya kuanza.
Wanane hao ni pamoja na beki wa kitambo wa timu ya Singida United Shafik Batambuze.
Wengine ni Pamoja na Washambulizi Nicholas Kipkirui na Erisa Ssekisambu and Erick Ogendo wanaotokea team za Zoo, Vipers na team ya vijana wadogo wa Gor Mahia mtawalia.
Viungo Erick Ombija na Kenneth Muguna pia wamejiunga na timu. Beki Pascal Ogweno amejiunga na timu kutoka Kariobangi Sharks naye Geoffrey Ochieng ambaye ni beki wa Kushoto amejiunga na Gor Mahia kutoka team ya Western Stima.
Wachezaji wapya
Erick Castro Ombija (Kenyatta University ), Erick Ogendo (Gor Youth), Erisa Sekisambu (Vipers SC), Geoffrey Ochieng (Western Stima), Shafik Batambuze (Singida United), Kenneth Muguna (FK Tirana), Nicholas Kipkirui (Zoo FC), Pascal Ogweno (Kariobangi Sharks)