Jose Mourinho kuturudisha kwenye vitabu vya Rekodi Januari
Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United yenye makazi yake katika jiji la Manchester nchini England, Jose Mourinho wakati timu yake ikiendelea kupambania nafasi ya kuingia TOP 4, Jose Mourinho ameanza kuhusishwa kutupia macho katika dirisha dogo la usajili ili kuboresha kikosi chake.
Kabla ya usajili wa majira ya joto kufungwa Jose Mourinho alinukuliwa na vyombo vya habari akimtuhumu wazi wazi mtendaji mkuu wa klabu hiyo Mr Ed Woord kutokamilisha baadhi ya mapendekezo yake muhimu katika usajili, sasa ameonekana kuanza tena harakati za usajili.
Jose Mourinho kwa sasa amekuwa akihusishwa kwa karibu kuhitaji saini ya beki wa Napoli ya Italia Kalidou Koulibaly ili kuimarisha safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo Mourinho amekuwa haridhishwi nayo sana katika michezo kadhaa.
Hata hivyo dili hilo lililoripotiwa na mtandao wa Mirror inaelezwa kuwa kuna uwezekano wa usajili huo kukamilika mwezi Januari 2019 lakini Mourinho kutokana na uhitaji wake wa dhati wa Kalidou Koulibaly katika kikosi chake yupo radhi pia kusubiri hadi mwisho wa msimu kama Napoli hawatokuwa tayari kumuachia mchezaji huyo raia wa Senegeal.
Kama usajili wa Kalidou Koulibaly ukimalika kwa dau la pauni milioni 89 kama inavyoripotiwa na baadhi ya mitandao, basi beki huyo ndio atakuwa mchezaji ghali zaidi duniani katika nafasi ya ulinzi, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Virgil van Dijk wa Liverpool kwa uhamisho wake wa dau la pound milioni 75 akitokea Southampton na kujiunga na Liverpool, kwa upande wa Koulibaly mwenye umri wa miaka 27 anajiongezea thamani yake kutokana na kucheza game 16 hadi sasa akiwa na Napoli akiwa hajaruhusu goli, akitoa pasi moja ya usaidizi wa magoli na ameoneshwa kadi tano za manjano.