Superclasico yaahirishwa tena
Rais wa shirikisho la soka America kusini CONMEBOL Alejandro Dominiguez amethibitisha mechi ya Superclasico ya marudiano ya fainali ya Copa Libertadores imeahirishwa kufuatia wachezaji wa Boca Juniors kuwepo katika hali mbaya kutokana na tukio la jana.
Mechi hiyo ya wababe hao wawili, River Plate na Boca Juniors ilipangwa kuchezwa leo baada ya kuahirishwa jana Novemba 24 kutokana na basi la wageni Boca Juniors kupigwa na mashabiki wa Riverplate wakati likiingia uwanjani na kusababisha kuumia kwa wachezaji wa Boca Juniors, wawili wakipelekwa hospitali.
Siku zijazo shirikisho hilo litaamua wapi na lini mechi hiyo ya marudiano itapigwa.
Mechi ya kwanza iliishwa kwa sare ya 2-2.