Nani alisema Yanga hawashindi nje ya Dar
Ligi Kuu Soka Tanzania Bara imeendelea leo kwenye Uwanja wa kaitaba huko Kagera kwa wenyeji Kagera sugar kupigwa mabao 2-1 na Yanga.
Yanga walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 21 kupitia kwa Heritier Makambo raia wa Kongo na baadaye Kagera kusawazisha kwa njia ya penati ikiwa ni dakika ya 32 kupitia kwa Ramadhan Kapera.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Yanga na Kagera wote walikuwa wametoshana nguvu kwa sare ya 1-1.
kipindi cha pili Yanga waliongeza kasi za mashambizi ya kusaka bao la kuongoza na katika dakika ya 74 Raphael Daud alifanikiwa kutikisa nyavu za Kagera kwa njia ya kichwa.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikia alama 32 kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi huku Azam akiwa kileleni na 33 na Simba aliye nafasi ya tatu akiwa na 27.
Kagera Sugar, wanapoteza mchezo wao wa 3 kwenye Ligi kuu wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani na kuwafanya wabaki na pointi 17.