Serie A waonesha mapenzi yao kwa wanawake.
Wachezaji wa Serie A jana walikuwa wamepaka rangi nyekundu katika nyuso zao ikiwa ni njia ya ku-support kampeni ya kuzuia unyanyasaji dhidi ya wanawake
Na katika mechi za leo na kesho jumatatu pia wachezaji, waamuzi katika ligi hiyo watafanya hivyo.
Hii ni njia mojawapo ya kusambaza elimu na uelewa kwa watu duniani kuhusu kuzuia unyanyasaji kwa wanawake
Leo Novemba 25 ndio siku ya kimataifa ya kuondoa unyanyasaji dhidi ya wanawake “ International Day for the Elimination of Violence against Women “